VIJANA SILAHA YA UCHUMI
Photo courtesy
Vita vya nchi kwa nchi pia vimesababisha kuzorota kwa uchumi, ikiwa kati ya nchi hizi ni wazalishaji wakubwa wa bidhaa za vyakula. Vita vya nchi ya Russia na Ukraine vimeathiri saana ukuaji wa uchumi humu nchini haswa Russia wakiwa wasambazaji wakuu wa bidhaa za mbolea na virutubisho humu nchini. Ni mwaka sasa tangu vita vianze na baadhi ya bidhaa hizo zilisimamishwa kusambazwa. Hali hii imesababisha kuzorota wa kilimo na uzalisha wa bidhaa za mashambani kwa jumla.
Utumizi mbaya wa fedha za serikali pia umepelekea kuzorota kwa hali ya kiuchumi nchini. Viongozi wengi wamekuwa wakitumia mamlaka yao kuvuja fedha za umma kwa mahitaji yao ya kibinafsi. Kwa kipindi cha miaka mitano kwenye uongozi wa aliyekuwa Rais wa hatamu ya nne Uhuru Kenyatta mabilioni yameweza kuvujwa kwenye wizara mbali mbali kwa kutoa zabuni bandia, kununua bidhaa hewa na kujipalilia mishahara mikubwa mikubwa. Pia kumekuwa na tabia ya viongozi wengi, watu mashuhuri na baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa hayatoi ushuru kwa serikali. Ukopaji wa fedha kutoka nchi za nje pia umesababisha kuzorota kwa uchumi chini. Viongozi wanarundikia nchi madeni ya fedha za mabilioni hali inayosababisha kudaiwa.
Photo courtesySerikali inafaa kuendeleza kampeni kwa vijana kuwahimiza kutoa ushuru. Vijana wengi kote nchini hawajaelimishwa manufaa ya utoaji ushuru hivyo kupelekea wengi kuhepa ulipaji wa ushuru. Amani pia kigezo kingine cha kuimarisha uchumi nchini. Vijana wengi mara nyingi ndio hutumika kuvuruga amani. Serikali pia inafaa kubuni kampeni za kuendeleza amani kwa vijana na kuvumisha maendeleo miongoni mwa vijana.
Vijana ndio mabarobaro wachapakazi na idadi kubwa hawana ajira. Serikali inafaa kubuni njia za kunufaisha vijana na kazi ili kuinua uchumi kote nchini.


Kaz mbashara
ReplyDeleteVijana ni Viongozi Wa Leo Na Kesho
ReplyDeleteNice
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteKuntu kaka
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete🔥🔥🔥
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteNakala nzuri.
ReplyDelete🔥🔥
ReplyDeletehongera
ReplyDeleteKazi nzurii
ReplyDeleteSafi
ReplyDeleteNzuri kaka
ReplyDeleteKazi safiii
ReplyDeleteSwadakta
ReplyDeleteKazi kuntu
ReplyDeleteUnefanya utafiti mzuri. Kazi nzuri
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKazi nzuri
ReplyDelete