HATUA ZANGU CHUONI
Safari huanza kwa hatua moja baada ya nyingine, kutoka mwanzo hadi kileleni. Safari hueza kuzongwa na milima na mabonde. Uvumilivu, bidii pamoja na matumaini humwezesha yeyote kukamilisha safari yake. Haijalishi ni safari gani, safari yoyote yaeza kuwa ya kawaida, kutoka eneo moja la kijiografia hadi linguine au safari ya hali ya kimaisha. Kama himizo kwa kila mtoto yeyote anayezaliwa duniani, nia ya wazazi wake ni kumlea vyema, kwenye maadili mazuri na zaidi kuimarisha ukuzi wake na zawadi ya elimu ya kimaisha na darasani. Pindi unapoianza safari hii kwenye hatua ya chini, shule ya chekechea tumaini la mzazi ni mtoto wake kufika kileleni mwa masomo yake. Kilele chake kikiwa chuo kikuu na kusomea taaluma bora zenye thamani. Kwenye makuzi yangu ningali mdogo shule ya msingi ya Brainsgate nilikuwa na lengo la kujiunga na chuo kikuu na kujikita na taaluma ya uanahabari. Nilijizatiti na kujitahidi masomoni na hatimaye ndoto yangu ilitimia na kuamka nikiwa chuo kikuu cha kiufundi Cha M...



