UKAME NA NJAA

 

Photo Courtesy 

Kadri siku zinavyoenda ni vigumu kupuuza ukweli uliopo kwamba halo ya hewa ulimwenguni kote inazidi kuwa isiyotabirika na mbaya zaidi. Hali hii imeleta dalili duniani kote na hata kujitokeza kwenye nchi mbalimbali barani Afrika. Kutokana na mabadiliko ya Hali ya hewa, kumeonekana uingezekaji wa viwango vya maji na kupelekea mafuriko yaletayo madhara makubwa, vipindi vya ukame vinakuwa vya muda mrefu na vyenye kujirudia mara kwa mara.

Mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yameleta na yanazidi kuleta athari nyingi kote duniani yamekuwa donda sugu. Mabadiliko haya yanasababishwa na uzalishaji wa gesi chafu kutoka kwenye viwanda mbalimbali. Gesi hii huifunika dunia na kunasa joto la jua hali inayopelekea ongezeko la viwango vya joto duniani na mabadiliko ya hewa. Wanasayansi wamekuwa wakiripoti mara kwa mara ongezeko kubwa la joto hali inayozidi kushuhudiwa na kila binadamu.

Uzalishaji wa umeme kupitia kuchomwa kwa nishati ya kisukuku kama vile makaa ya mawe, mafuta na gesi asilia imesababisha kuathirika kwa hali ya hewa ulimwenguni. Kutokana na taarifa iliyochapishwa na shirika la NASA mwaka 2021 ilionyesha umeme mwingi bado unazalishwa kutokana na nishati ya kisukuku. Hali ingine inayosababisha ubadilikaji wa hali ya hewa ni ukataji wa misitu kwa minajili ya kutenga mashamba na malisho au makazi. Hali hii husababisha ukuaji wa hewa chafu kwani miti inapokatwa hutoa kaboni ambayo imekuwa ikiihifadhi aghalabu hali hii huzuia uwezo asilia wa kutengeneza hewa asili kutoka kwa anga hewa.

Photo Courtesy 

Kati ya madhara yanayoletwa na ubadilikaji wa hali ya hewa nchini Kenya ni kuongezeka kwa joto na ukame wa mara kwa mara. Hali hii imedhihirika kwenye baadhi ya sehemu nyingi kama Turkana, Marsabit, Wajir, Samburu na baadhi ya sehemu za pwani; Kilifi, Tana River na Kwale. Athari za upotevu mkubwa wa mazao na mifugo ziletazo njaa, kuhama makazi na vitishio kwa afya na ustawi wa binadamu vimeonekana. Binadamu wengi pamoja na wanyama wamepoteza maisha halikadhalka  ubadilikaji wa hali ya hewa umeleta kushuhudiwa mafuriko makubwa kote nchini, mashambani na hata mijini na athari zimeonekana chungu nzima ikiwemo kupoteza mifugo na mimea.

Madhara yote ya ubadilikaji wa hali ya hewa nchini yanaweza kusuluhishwa na upandaji wa miti zaidi kote nchini na sheria zizidi kutiliwa mkazo za ukataji wa miti ovyo. Kilimo kinachozingatia hali ya hewa kiimarishwe. Wananchi wafundishwe ni mimea gani wanafaa kupanda na wakati gani haswa. Halmashauri iundwe ya kufuatilia uendelezaji wa nishati ya joto, ardhi na safi. Hii itarudisha na kuimarisha hali halisi ya hewa safi kote nchini. Kamati kuu iweze kuundwa na serikali ya kufuatilia udhibiti wa hali ya ukame kote duniani.

Comments

  1. Kuna haja ya sisi wakenya kujitahidi kusuluhisha jambo hilo
    Kazi safi

    ReplyDelete
  2. Wooow Napenda hiii kazi safi mkuu

    ReplyDelete
  3. Kazi safi kaka. Good choice of pictures

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts