UHURU WA BANDARI PWANI.

 

Photo Courtesy: Kenya Ports Authority

Kufuatia kuhamishwa kwa baadhi ya shughuli za bandari kuu ya Mombasa hadi Naivasha mwaka wa 2015 kuliendelea kuripotiwa malalamishi mengi kutoka kwa wananchi haswa wakaazi wa mji mkuu wa Mombasa, wanaofaidi moja kwa moja kutoka kwa bandari ile.

Baadhi ya shughuli zilizoweza kuhamishwa moja Yao ilikuwa sehemu ya kuhifadhi makashani na ya pili ilikuwa Ni ofisi za kusafisha na kusambaza mizigo bandarini.

Photo Courtesy: Kenya Ports Authority 

Walioripotiwa kuathirika zaidi walikuwa ni wenye mijengo iliyosheheni ofisi hizi,wachuuzi wa vyakula,madereva pamoja na ushuru kwa kaunti.Taasisi iliyofaidika zaidi ilikuwa Ni reli ya usafirishaji mizigo kutoka bandarini Hadi Naivasha. mnamo tarehe 13 Septemba hatimaye nuru ilionekana kwa wakaazi wa Mombasa na pwani kwa jumla. 

Hii ilikuwa baada ya Rais William Ruto kitimiza ahadi aliyokuwa amewaahidi wapwani ya kirudisha shughuli za bandari mjini Mombasa.Kwa sasa baadhi ya shughuli hizo zinafanyika mjini na wakaazi wa Mombasa walifurahishwa na jambo hili. Uchumi wa kaunti ya Mombasa inatarajiwa kuimarika zaidi. 


Comments

  1. Bandari ya Mombasa ndio kitovu cha wapwani
    Kazi nzuri kaka

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts