VIJANA SILAHA YA UCHUMI

 

Photo courtesy 
Kutokana na ubadilikaji wa hali ya kimaisha duniani umechangia kuzorota kwa uchumi kwenye nchi tofauti tofauti hapa duniani. Mojawapo ya hali zilizochangia kushuka kwa uchumi ni ubadilikaji wa hali ya anga iliyosababisha nchi nyingi kuathiriwa na ukame aghalabu kusababisha kutokupatikana kwa vyakula kwenye mashamba haswa humu nchini sehemu kadha zimeweza kuathirika na ukame hali iliyosababisha baa la njaa. Sehemu hizi zikiwemo kazkazini, mashariki na pwani ya Kenya.

Vita vya nchi kwa nchi pia vimesababisha kuzorota kwa uchumi, ikiwa kati ya nchi hizi ni wazalishaji wakubwa wa bidhaa za vyakula. Vita vya nchi ya Russia na Ukraine vimeathiri saana ukuaji wa uchumi humu nchini haswa Russia wakiwa wasambazaji wakuu wa bidhaa za mbolea na virutubisho humu nchini. Ni mwaka sasa tangu vita vianze na baadhi ya bidhaa hizo zilisimamishwa kusambazwa. Hali hii imesababisha kuzorota wa kilimo na uzalisha wa bidhaa za mashambani kwa jumla.

Utumizi mbaya wa fedha za serikali pia umepelekea kuzorota kwa hali ya kiuchumi nchini. Viongozi wengi wamekuwa wakitumia mamlaka yao kuvuja fedha za umma kwa mahitaji yao ya kibinafsi. Kwa kipindi cha miaka mitano kwenye uongozi wa aliyekuwa Rais wa hatamu ya nne Uhuru Kenyatta mabilioni yameweza kuvujwa kwenye wizara mbali mbali kwa kutoa zabuni bandia, kununua bidhaa hewa na kujipalilia mishahara mikubwa mikubwa. Pia kumekuwa na tabia ya viongozi wengi, watu mashuhuri na baadhi ya makampuni ambayo yamekuwa hayatoi ushuru kwa serikali. Ukopaji wa fedha kutoka nchi za nje pia umesababisha kuzorota kwa uchumi chini. Viongozi wanarundikia nchi madeni ya fedha za mabilioni hali inayosababisha kudaiwa.

Photo courtesy 
Vijana wanafaa kuwa kwenye mstari wa mbele kurudisha hali ya uchumi kuwa sawa. Zipo hatua pendekezi ambazo vijana wanaweza kutumia kuimarisha uchumi nchini. Vijana wanafaa kufadhiliwa na mikopo ya kujiendeleza kibiashara, haswa tatizo kubwa likiwa ukosefu wa ajira. Serikali inafaa kueka mikakati ya kuinua vijana kwa kubuni nafasi za kazi kupitia kujenga viwanda tofauti tofauti kote nchini.

Serikali inafaa kuendeleza kampeni kwa vijana kuwahimiza kutoa ushuru. Vijana wengi kote nchini hawajaelimishwa manufaa ya utoaji ushuru hivyo kupelekea wengi kuhepa ulipaji wa ushuru. Amani pia kigezo kingine cha kuimarisha uchumi nchini. Vijana wengi mara nyingi ndio hutumika kuvuruga amani. Serikali pia inafaa kubuni kampeni za kuendeleza amani kwa vijana na kuvumisha maendeleo miongoni mwa vijana.

Vijana ndio mabarobaro wachapakazi na idadi kubwa hawana ajira. Serikali inafaa kubuni njia za kunufaisha vijana na kazi ili kuinua uchumi kote nchini.

Comments

  1. Vijana ni Viongozi Wa Leo Na Kesho

    ReplyDelete

Post a Comment