SUMU INAYOWAMALIZA WANAFUNZI VYUONI

 


Mahusiano ya kimapenzi huhusisha sana watu wa umri mdogo hadi wa kati. Kutokana na kubadilika kwa ya hali ya kimaisha mahusiano haya yamechanganisha vijana wadogo na watu wa umri mkubwa wa hadi miaka zaidi ya hamsini. Asilimia kubwa ya watu duniani kote wapo kwenye mahusiano au wamewahi kujikuta kwenye mahusiano ya kimapenzi. Wengi hujiuliza mpenzi ni mtu wa aina gani na mapenzi haswa huendelezwaje? Mpenzi ni yule atakayekuonyesha upendo wa dhati. Kulingana na mwanafalsafa Jhidhu Krishna Marti binadamu kwenye mahusiano huongozwa na matamanio na msimamo wake huwa ni wa kibinafsi zaidi. Binadamu atakupenda ikiwa tu utatimiza mahitaji yake, kama humtimizii anachokihitaji basi kamwe haezi kukupenda.

Vijana wengi kwenye vyuo vikuu kote nchini wamejitosa kwenye mapenzi wengi wao wakiwa na matumaini ya kuoana baadaye na baadhi yao wakiyachukulia mahusiano kama hali ya kujiliwaza na kufurahisha nafsi zao. Watafiti wanasema unapopenda zaidi hua si rahisi kujinasua, ni kama mtego. 



Mahusiano ya wanafunzi wa vyuo vikuu huzongwa na mabonde mengi yasiyopandika wala kuteremkia ikiweno usaliti na kutotimiza wajibu kama mpenzi. Hali hii husababisha msongo wa mawazo miongoni mwa wanafunzi na kuwapelekea wengi wao kujitosa kwenye matumizi ya madawa ya kulevya na wengine kufanya vitendo vya ajabu kama kujitoa uhau. Wengine watalalamikia msongo wa mawazo na kuwasababishia kudhoofika kiafya na hata kuathiri shughuli zao za kawaida. 

Wito unazidi kutolewa na wanafalsafa na washauri wa mahusiano ya kimapenzi, endapo utajipata kwenye hali kama hii kutendwa au kusalitiwa unashauriwa kukubali yalikujiri na kuanza kusonga mbele. Pia unashauriwa kutafuta ushauri ili kukupunguzia mzigo huu.


Comments

  1. Wazii jeshi๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ

    ReplyDelete
  2. Nakala safi kaka๐Ÿ‘๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  3. Ukweli mtupu mapenzi nikama mtego tu hukushika hadi wakati mwingine hujatarajia daahh

    ReplyDelete
  4. ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚this one though. Good job

    ReplyDelete
  5. Kiswahili kitukuzwe๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ’ฏ

    ReplyDelete
  6. ๐Ÿ˜‚ Mswazi Wetu ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ

    ReplyDelete
  7. Kiongozi men deserve something ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

    ReplyDelete
  8. This is hilarious ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿ’ฅ๐Ÿ’ฅ

    ReplyDelete
  9. Mapenzi hayataki haraka!

    ReplyDelete
  10. Kweli kabisaa ๐Ÿ˜‚๐Ÿ’ฏ

    ReplyDelete
  11. Ukweli mtupu๐Ÿ’ฏ๐Ÿ’ฏ

    ReplyDelete
  12. kazi nzuri๐Ÿ‘๐Ÿ‘

    ReplyDelete
  13. Kaka nakuaminia since day one

    ReplyDelete
  14. Ukweli uchungu๐Ÿ˜‚

    ReplyDelete
  15. Hakuna mapenzi ya shuleni na Kama ipo, ni moja kati ya mamilioni. Kazi safi bro

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular Posts